Posted on 2018-04-04 11:53:36

Na.Alfeo Mbunji

Tume huru ya uchaguzi ya chuo cha uandishi wa habari Morogoro Msj, imetangaza rasmi tarehe ya uchaguzi ambapo awali  ulihairishwa baada ya wagombea kukosa sifa stahiki.

Akizungumza na Msj Online  mwenyekiti  wa tume hiyo Bw.Frank Damas, amesema kuwa ratiba iliyotoka itakamilisha mchakato mzima wa kuchagua viongozi watakao ongoza serikali ya wanafunzi ya chuo cha uandishi mororogo msj siku za mbele

’’Ratiba tumetoa ambayo inaonesha wazi kwamba uchaguzi unakamilika wiki hii hivyo wanafunzi wajaindae kupiga kura  siku ya alhamisi ya tarehe april 2018’’alisema Damasi

Aidha kwa upande wao wanafunzi wa chuo hicho, wameishukuru  tume ya uchaguzi kwa kutoa ratiba na mchakato mzima wakumtafuta kiongozi huku wakiomba uchaguzi kuwa  wa  huru na wa haki

’’Toka mwanzo wa mchakato wa uchaguzi tume imetupa taarifa ila tunaiomba tume Ikamilisha mchakato wa uchaguzi kwa uhuru na  haki kama jina lao la tume ya huru na haki’’Waliongeza wanafunzi wakizungumza na Msj Online katika nyakati tofauti

Wanafunzi wa  chuo cha uandishi wa habari morogoro wanatarajia kufanya uchaguzi kwa nafasi ya urais ;a makamu wa urais siku ya alhamis ya wiki hii April 05 2018