Posted on 2018-03-07 01:09:21

Kuna msemo unasemwa sana ukitaka kumficha mwafrika weka ujumbe kwenye kitabu wakimaanisha watu weusi hatuna tabia ya kupenda elimu,tunapenda vitu rahisi,  tunapenda shotcut labda kulingana na mazingira tumeyokua na kuyakuta lakini michezo inaweza kua chachu kwa namna moja au nyingine ya vijana kupenda kusom na kutamani kua shule   Watoto hupenda kua na furaha, nani asiejua kua mfumo wa elimu yetu haumfanyi mtoto kua na furaha
anapokua shuleni?pengine labda shule za kisasa (English Medium) ambazo hulipisha fedha nyingi  lakini

hizi za kawaida ambazo wengi wetu ndio tumesoma hazimfanyi mtoto kufurahia mazingira ya shule au vyuo vyetu hivo michezo hua sehem ya burudani kwa mtoto anapokua na uhakika kua baada ya masomo atapata wasaa wa kucheza michezo mbalimbali itamfanya mtoto kupenda shule

 Watoto wanapenda kua na marafiki wapya kwa kiasi fulani michezo humfanya mtoto kukutana na marafiki wapya mfano kulipokua na mechi ya kirafiki kati ya Chuo cha Uandishi wa Habari Morogoro na jirani zao wa TASO ilikua fursa nzuri kwa vijana hao kutengeneza marafiki wapya hivo kwa namna moja kijana anaependa michezo siku hio alikuja chuo ili baadae apate nafasi ya kwenda kwenye michezo hio

Watoto wenye vipaji huhitaji sehem ya kuonesha vipaji vyao hivo wanapokua mashuleni sehem sahihi kwao ya kuonesha vipaji vyao katika michezo mbalilmbali ni shuleni ikiwa tu kuna mazingira mazuri kwa wao kufanya hivo,jambo hilo huwafanya watoto hata kama mazingira ya shule hayako vizuri wapende kujisomea wakiamini pamoja na kupata elimu watapata nafasi ya kuonesha vipaji vyao mfano katika chuo cha uandishi wa habari morogoro kulikua na kijana mmoja aliepata kuitwa swedi namuntu,alikua nakipaji kikubwa cha kucheza soka kipindi chuo hiko kilipokua na kalenda nzuri ya michezo hasa mechi za kirafiki  dhidi ya taasisi za jirani alikua mhudhuriaji mkubwa sana wa masomo yake lakini baada ya chuo hiko kupuuzia michezo mahudhurio yake yakishuka hatimae kuacha kabisa chuo

          Pengine chuo hiko kilipoteza mwanahabari mzuri mwenye kipaji cha kandanda ambacho labda siku moja angekuja kuisaidia timu yetu ya taifa ambayo inasua sua katika mashindano ya kimataifa  wakati kulikua na njia ya kumfanya apende na kuthamini chuo kwa kua tu na kalenda nzuri ya michezo chuoni hapo

         Michezo huongeza uwezo wa kufikiri wa mtoto,hili halipingiki kua mtoto mwenye furaha n aNejitahidi shuleni lazima apende shule kufeli au kutofanya vizuri shuleni hua sababu mojawapo ya mtoto kuchukia shule lakini wanasayansi Karibia wote wanakiri mtoto anaependa michezo hua na uwezo mkubwa wa kufiiria ukilinganisha na mtoto ambae hapendi michezo hivo kumfanya apende shule kwa sababu kwanza atajitahidi na kukwepa ile fedheha ya kuitwa “kilaza”

 

Na Zulpha Mbwambo