Posted on 2018-02-27 14:36:43
Mapema ya Oktoba 28, 2017 baadhi ya Wanafunzi na mlezi wa Wanafunzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari Morogoro (msdis) Francis Mkude walitembelea kituo cha Watu wenye Ulemavu wa akili THE SOCIETY OF MEHAYO kinachopatikana Mazimbu, Manispaa ya Morogoro.
.
Ujumbe huo kutoka msdis ulikwenda kituoni hapo kwa lengo la kuwatembelea na kukabidhi michango iliopatikana baada ya kuchangishwa na Wizara ya Dini na Mahusiano kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais ya Chuo hicho.
.
Pia kituoni hapo jumbe huo kutoka msdis ulipata nafasi ya kusaidia kazi za mikono na baadae kuhitimisha kwa kucheza michezo tofauti na watu hao wenye ulemavu wa akili.